Inatafuta...

Picha za Instagram za watoto wa afisa wa polisi wa Kenya wakila bata na ndege ya jeshi zazua utata!

Picha zilizowekwa Instagram za wasichana wakiwa wamekaa pembeni ya ndege ya polisi iliyokuwa itumike kuwabeba maofisa wa Recce kwenda kukabiliana na shambulio la Garissa zimezua utata nchini Kenya.

Picha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya Instagram ya Ndanu Munene Mbithi, anayesemekana kuwa binti wa polisi wa anga wa Kenya, Kamanda Rogers Mbithi.

Picha hizo zinamuonesha Ndanu akiwa na msichana mwingine kwenye matukio tofauti, moja ikiwa ni wiki 10 zilizopita na nyingine wiki 62 zilizopita.

Picha mbili zimeandikiwa maelezo, “Mombasa ni raha tu.” Na nyingine ya msichana akiwa ndani ya ndege hiyo iliyoweka 27 zilizopita imeandikiwa, “Hi Mombasa. #birthdayweekend.”

Akaunti hiyo ya Instagram iliyounganishwa na Twitter na Facebook kwa jina la Ndanu Mbithi imefutwa jana tangia picha hizo ziwekwe hadharani.

Wakenya wenye hasira jana walihoji kuhusiana na matumizi mabaya ya ndege za polisi na kwanini akaunti hizo zilifutwa.

Weekend iliyopita ilibainika kuwa ndege hiyo ya Cessna iliyokuwa iwapeleke makomando wa kikosi cha Recce hadi kwenye chuo kikuu cha Garissa hakupatikana kwakuwa ilikuwa imeenda Mombasa kwa safari binafsi bila ruhusa wa IGP.

IG Joseph Boinet amethibitisha kupokea ripoti inayothibitisha kuwa ndege hiyo haikuwepo kwakuwa ilikuwa Mombasa kupeleka watu. Ndege hiyo iliondoka Nairobi April 2 saa 1.30 asubuhi ikiwa ni masaa mawili baada ya shambulio la kigaidi kwenye chuo kikuu Garissa.

Ndege hiyo ilidaiwa kukodishwa na maafisa wa juu wa polisi kwa mfanyabiashara wa Nairobi kwa maelekezo kutoka kwa Mbithi kwenda kumchukua mke wa mtoto wake.

Shahidi Aeleza Kisa cha Al Shabaab Kuuwa Wasichana Wengi Katika Shambulio la Kigaidi Chuo cha Garissa Kenya

A survivor of the deadly terror attack in Garissa University has told the media how the Al Shabaab tricked female students to draw them out in the open and kill them like insects.

Narrating his story, Francis Gicobi, a second year Bachelor of Education student, said many female students fell for Al Shabaab’s lies and that’s why they were killed in large numbers compared to male students.

Gicobi noted that when Al Shabaab stormed the women’s hostel, they tricked them to comply with their orders to come out because they would not be killed since Islam does not permit them to kill women.

Many females students fell for this lie and came out and the Al Shabaab sprayed them with bullets indiscriminately killing them like insects

The Al-Shabaab shouted 

“Kama hamtaki kufa, tokeni hapa nje nyote kwani kulingana na dini yetu, hatuui wasichana na kwa hivyo mtoke taratibu kwa gorofa hadi hapa chini, au mpigie baba zenu simu waje wakuokoe. (If you don’t want to die, come outside. According to our religion, we do not kill girls. Walk down the stairs to the ground level, or alternatively call your fathers to come and save you),” narrated Gicobi.

“Female students walked to the ground floor of the storied building in droves only for the attackers to indiscriminately spray them with bullets,” he added.

However, he thanked God for keeping him alive to tell Kenyans what he witnessed on that fateful day.

“I thank God for saving me to be able to tell Kenyans what I witnessed as my innocent colleagues were riddled with bullets like animals,’’ he said.

Video: Mwanafunzi Wa Kike Ajiyejificha Ndani Ya Kabati Kwa Saa 48 Wakati Wa Shambulizi La Chuo Kikuu Cha Garissa Akila 'Lotion' Asimulia Mkasa Mzima

Mwanafunzi wa kike aliyejificha ndani ya kabati kwa saa 48 wakati wa shambulizi la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya hatimaye amejitokeza.Msichana huyo anasema kuwa alitumia mafuta aina ya 'lotion' kama chakula ili aweze kuishi..

Davido Apost Picha Akiwa na Diamond Studio na Kuandika Ujumbe Uliotuacha njia Panda!

Uhusiano kati ya Davido na Diamond Platnumz ulishavunjika siku nyingi kufuatia issue iliyotokea mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big Brother Africa.


Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi

Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo mpya Davido kwenye Instagram.

Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm this album yo.”
~Bongo5

Kijana Henry Chau achinja familia yake na kuwala Nyama.. Habari kaili iko hapa..



http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/04/01/150401055530_chau_kiliing_512x288_bbc_nocredit.jpg Henry Chau anayejiita mwendawazimu
Mwanamume mmoja raia wa Hong Kong amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji,kutawanya viungo vya nduguze ,kuwanyunyizia chumvi na kuwapika.

Mtuhumiwa huyo wa mauaji ya kushangaza ana umri wa miaka thelathini na mmoja jina lake ni Henry Chau aliibua hisia za walio wengi katika kesi ya namna yake mnamo 2013 wakati kichwa cha mamake mkubwa pamoja na babake vilipobainika kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.

Majaji wa mahakama kuu nchini Hong Kong ,wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea walisikiliza namna Chau alivyotekeleza mauaji yake ,kwanza huua, pili hutawanya viungo vya maiti na kisha huwanyunyizia chumvi ili kuongeza ladha ,na anasema yote hayo ni matokeo ya mapenzi yake kwa nyama choma ya kiti moto,na nyama hiyo ya binaadamu zikisha iva ama kuchomwa huwa anafunga nyama hizo katika makasha ya chakula paoja na ubwabwa,na polisi walipofanya upekuzi katika nyuma yake walikuta baadhi ya viungo katika chombo cha kuhifadhia taka.

Akitoa hukumu dhidi ya kesi hiyo,jaji Michael Stuart-Moore alimuelezea Chau kama mbinafsi mwenye msongo wa mawazo kutokana na mafanikio mabaya yake ya maisha na asiye na huruma kwa wengine.

Chau, alihukumiwa adhabu mara mbili kifungo cha maisha jela na miaka tisa namiezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa kuvunja sheria ya kuzika miili ya familia yake isivyo kawaida kosa ambalo alikiri baadaye.

Rafiki wa Chau anayehusishwa katika mauaji hayo alikutwa hana hatia mwishoni mwa wiki iliyopita .

Taarifa za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa ,Chau alidanganya kuwa jamaa zake walikwenda China,lakini baadaye alijisahau na kumuandikia rafikiye kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.

Chau mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia watu wake wa karibu na kusema kwamba hawezi kumuonea huruma mtu yeyote kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni mpaka anakuwa mtu mzima.Na alimua kuwadanganya polisi ilia pate wasaa wa kuwaaga marafiki zake.

Hinki ndio chanzo cha Chris Brown Kuwahamishia Mwanae na Mama Yake Nyumbani Kwake, soma hapa..

Chris Brown amepanga kumchukua mwanae pamoja na mama yake na kuishi nao nyumbani kwake, mtandao wa Hollywood Life umesema.

Chris Brown, 25, anataka mwanae wa kike mwenye umri wa miezi tisa, Royalty na mama yake, Nia Amey, 31 kuhama kutoka Houston wanakoishi sasa, ili waishi naye nyumbani kwake jijini Los Angeles.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoongea na mtandao huo, Chris anataka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka 26 akiwa na Royalty.

Chris anataka kuhakikisha kuwa anamuona mwanae kila siku.

Wanaigeria Wafanya Kweli Wakipiga Chini Chama Tawala na Kumchagua Raisi wa Upinzani..Story Kamili iko hapa...

Mgombea wa upinzani nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameibuka mshindi wa kiti cha urais dhidi ya Rais Goodluck Jonathan katika uchaguzi uliofanyika Jumapili nchini humo.

Kwa mujibu wa Reuters, Buhari wa chama cha upinzani cha APC amepata kura million 15.4 dhidi ya kura million 13.3 alizopata Jonathan.

Chama cha Rais Jonathan All Progressives Congress (APC) kimesema kuwa Jonathan amekubali matokeo na amempigia simu Buhari kumpongeza kwa ushindi huo.

Ushindi huu wa Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa jeshi unaandika historia katika taifa hilo kwa kuwa ni mara ya Kwanza kwa chama cha upinzani kushinda kiti cha urais kwa njia ya kidemokrasia

Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo wamepongeza namna uchaguzi ulivyoendeshwa licha ya kuripotiwa kwa hujuma katika baadhi ya maeneo ambazo zilisababisha hofu ya kutokea kwa vurugu.

Je, Tanzania tunapoelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba 2015 tujifunze nini kutoka katika uchaguzi huu?

Dillish: Hela Nilizoshinda Big Brother Afrika Zimekwisha Zote

Dillish Mathews, mshindi wa shindano la Big Brother Africa mwaka juzi, amedai kuwa amemaliza fedha zote alizoshinda.

Mrembo huyo wa Namibia aliyejishindia zaidi ya shilingi milioni 500 amepost video kwenye mtandao wa Instagram na kuongea maneno ambayo wengi wamechukulia kama utani kuwa hana tena fedha hizo.

“About what I did with my money that I got from Big Brother? It’s finished. A couple of Rolexes, kept going to Milan, London, Hong Kong, Shanghai…it’s finished. Kapu,” anasikika akisema kwenye video hiyo.

Kwenye video hiyo aliandika: Read on social media im broke… So here it is just in case your life depended on it. I don chop finish”

Hata hivyo wengi wamekerwa na kauli yake.

Afrika Magharibi yakoshwa na utamaduni wa mswahili uliooneshwa na Diamond kwenye video ya ‘Nasema Nawe’

Video hiyo inaonesha utamaduni wa mswahili wa pwani ambaye amerithi mambo mengi kutoka kwa waarabu.
Hivi ni vitu ambavyo Afrika na dunia nzima imevisoma kwenye historia ya ukoloni. Kupitia video na wimbo wake, Diamond amewapa mashabiki wa muziki wa Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na nchini zingine nje ya Afrika Mashariki, picha halisi ya maisha ya mswahili.
Taarab na mduara ni nyimbo zenye asili ya Tanzania na hivyo wimbo kama ‘Nasema Nawe’ inawakilisha kile tunachoweza kusema kwa kujigamba kuwa ni muziki wa Tanzania. Kitendo cha kumuongeza Khadija Kopa, malkia wa mipasho nchini, kimeuongezea thamani kubwa sana wimbo huo.
Nisisahau kusema kuwa Khadija Kopa na Hanscana wamewekwa kwenye sehemu ambayo sasa jicho la Afrika linawaona.
Hivi ni vitu vigeni kwa nchini kama Nigeria na Ghana. Hivi ni vitu ambavyo wasanii wao hawawapi kwasababu sio utamaduni wao. Ndio maana pamoja na kutoelewa Kiswahili, bado wamevutiwa na video na wimbo huo kwasababu wanasikia ladha mpya na kuona picha za tofauti.
“I dont understand a single word,but Diamond is honestly as his name says. Loyal fan from Namibia. #teamdiamond,” ameandika Rauha Vroutjie.
Jana jina la Diamond lilifanikiwa kushika namba moja kwenye trend topics za kwenye mtandao wa Twitter masaa machache tu baada ya kuachia video hiyo. Kwa msanii wa Tanzania kutrend Lagos, Nigeria si kitu cha kawaida, ni kikubwa.
Diamond amevuka hatua ya kuwa msanii maarufu Tanzania peke yake na kuwa msanii maarufu Afrika. Akishuka Luanda, Angola ama Gaborone, Botswana, hakuna shaka wengi watakuwa wanaifahamu sura yake.
Sehemu alipofikia ana uwezo wa kufanya wimbo wowote na Afrika ikamuelewa. Kutengeneza wimbo wenye vionjo vya Tanzania ni uamuzi mzuri zaidi alioufanya.
Kwahiyo msisitizo ninaopenda kuutoa hapa ni kwamba hatuwezi kuwashtua wanaijeria ambao kwa sasa ndio wameushikilia muziki wa Afrika, kama tukiiga muziki wao na kuwapa ladha ile ile wanayopewa na wasanii wao. Hawawezi kushtuka!
Hebu fikiria mfano huu. Kama wewe ni mkazi wa Bukoba na ukaja kumsalimia ndugu yako wa Dar es Salaam halafu chakula pekee atakachokupa kikawa ni ndizi, utajisikiaje? Umeziacha ndizi pomoni Bukoba halafu unakuja Dar unapikiwa ndizi tena? Tafakari.
Kwahiyo wasanii wanaopata bahati ya kuwashirikisha wasanii wakubwa wa Nigeria au Afrika Kusini, ili collabo zao zionekane za maana wanatakiwa kutengeneza nyimbo zenye ladha ya Tanzania ili kuwapa wapenzi wa muziki huo muziki tofauti.
Kwa wasanii ambao wamepata bahati ya kuwa na majina makubwa, kama wanataka kuchukuliwa serious, wahakikishe kama hawatengenezi nyimbo zenye mahadhi ya dunia (universal genres) ambazo ni pamoja na Hip Hop, R&B ama Pop, basi watengeneze nyimbo zenye ladha halisi ya Tanzania, yaani Bongo Flava.
Mtanzania akifanya Kwaito au muziki wa Naija nahisi kama hatofika popote.

Davido Awauzi Wakenya Vibaya Alipoenda Nchini Humo Kuburudisha Jumamosi iliyopita. Story Kamili Iko Hapa..

Today the theme is Davido. No artist has generated more hate from Kenyans in recent years than the Nigerian, and looking at the events of the past weekend, it’s clear why.

Davido started off his visit at NTV studios, and it was obvious he had no idea he was inside the largest media house in East Africa, perhaps even larger than any private media in Nigeria.

His pride and arrogance started when he met Victoria Rubadiri and Yvonne Maingi, and continued downstairs on Kimathi Street as he was being interviewed by Larry.

We have written extensively about that.

Read: Davido Angers Kenyans With His Arrogance on The Trend

Read: Hilarious Memes After Davido’s 20 Minutes Performance

On Saturday night, the Nigerian disappointed fans at Carnivore after giving a performance of less than 30 minutes. Below we have some reactions from Twitter.





Picha: Tizama Picha Ya simu Iliyo Tengenezwa Kwa Majani Bofya Hapa Kutizama Picha zake


Teknolojia inatufungulia mapya kila siku.. Nakumbuka simu za kwanza za mkononi zilikuwa kubwa halafu nzito, baadae ikaja fashion ya simu ndogo ndogo, zile kubwa watu wakawa wanaziita ‘mshindi’ ambalo ni jina la sabuni… Sasa hivi tunaona fashion ya simu kubwa inarudi mdogomdogo.

Sean Miles anaingia kwenye historia, anaingia kwenye headlines pia.. yeye kagundua hii simu ambayo imetengenezwa kwa majani kabisa pamoja na mchanganyiko wa vitu vingine vilivyochakaa ama vilivyoharibika.

O2-recycle-grass-phone-designboom03 
Dili ambayo alipewa na Kampuni ya O2 ilikuwa Miles afanye ubunifu njia ambayo wataweza kutumia mabaki ya vitu ambavyo vimechakaa na havifai kwa matumizi, katoka na hii ambayo hata waliomuagiza hiyo kazi imewashangaza yani.

Unaambiwa cover ya simu hii ukiiangalia ni kama majani kabisa.

_81927339_grassphone2 
Ubunifu huu umefungua ukurasa mpya kwenye Teknolojia, Kampuni ya O2 wanaangalia kama wataweza kuweka nguvu nyingi zaidi ili simu zenye cover hizi zilizotengenezewa majani zitengenezwe nyingi na kuingia kwenye soko la Dunia.

O2-Grass-Phone-31-537x444

Vipi mtu wangu ukikutana na hii simu pale Kariakoo an Mlimani City kuna kitu kitakufanya usiipende labda?

Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi ya taifa India.

Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini India.
Kulingana na vitabu vya kumbukumbu ya rekodi za taifa, Dolly Shivani Cherukuri kutoka Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh aliweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kusajili alama 200 katika mashindano yaliyoandaliwa jumanne iliyopita.
Kulingana na jarida la Press Trust la India ,mtoto huyo alifuma mishale 36 kutoka umbali wa mita 5 na kisha umbali wa mita 7 na kujizolea alama 388.
Tukio hilo lilishuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.''kwa hakika tunajivunia matokeo haya ''alisema afisa wa shirikisho la mishale la India bwana Gunjan Abrol.
Dolly ambaye alizaliwa baada ya kupandikizwa kwa mbegu ya babake kufuatia kifo cha kakake katika ajali ya barabarani. 
Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India.Kakake alikuwa mrushaji mishale wa kimataifa Cherukuri Lenin.
Babake Cherukuri Satyanarayana ,anasema kuwa Dolly alifunzwa kufuma mishale, tangu alipozaliwa.
Babake ni mmiliki wa klabu kimoja kinachofunza kurusha mishale.
Aidha aliiambia shrika la habari la AFP kuwa kitambo alikuwa amemptengezea uta na mishale nyepesi ilikukuza talanta ya mtoto huyo.
Sasa babake anasema kuwa anapanga kumshirikisha mwanawe katika mashindano kwa nia ya kumsajili katika vitabu vya rekodi za dunia za Guinness.
BBC

Yasemekana Rubani Wa ndege ya Ujerumani Iliyo Paata Ajali Ufaransa Aliiangusha Ndegehiyo Makusudi. Story Kamili Iko Hapa...

 Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.
 Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege. Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.




 Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea. Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari

ANGELINA JOLIE AFANYIWA UPASUAJI, ATOLEWA OVARI, MIRIJA YA UZAZI

Angelina Jolie.
MWIGIZAJI wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie amelazimika kutoa ovari zake pamoja na mirija ya uzazi baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.
Angelina Jolie, mumewe Brad Pitt wakiwa na watoto wao.
Staa huyo maarufu wa Hollywood amelidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa viungo hivyo wiki iliyopita katika upasuaji wa dharura.
"Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani" alisema Jolie
Habari hizi zimewashtua mashabiki wa mrembo huyo ambaye miaka miwili iliyopita alilazimika kukatwa titi kwa sababu ya tishio hilo hilo la Saratani.
Angelina Jolie akiwa na mumewe Brad Pitt.
Mama mzazi wa staa huyo aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.
"Siyo jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu" aliongeza Jolie.
Jolie ambaye ni mke wa mwigizaji nyota wa Holywood, Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.
Mastaa hao wana watoto sita ambapo kati yao wengine ni wakuhasili.

>>2jiachie

[PICHAZ] Yule Binadamu Mrefu Kuliko wote Duniani Kakutana Na Mfupi Kuliko wote Duniani Picha Ziko Hapa..



Binadamu Mrefu na Mfupi Kuliko wote
Hizi Ni baadhi ya picha za kijana mrefu kuliko wote duniani Aliyokutana na mfupi kuliko wote duniani

Davido Atembea Barabarani akiwarushia hela Shabiki wake.. Picha ziko hapa

kwa kweli on this mwanamusic davido amechemka to me throwing the money to the street like slavery kwa kweli hii haijakaa poa, leo kupitia mtandao wake wa jamii mwanakaka davido mara baada ya kuchkua degree yake na kurejea nchini alipost video akionyesha mashabiki wake wakiwa na furaha wakimsubiria airport, but kitendo kilichowasitikisha wadau wengi wa musiki ni pale pindi mwanakaka huyo alipoaanza kuzirusha hela barabarani huku gari likitembea na wananchi wakianza kuziokota kiukweli to me kitendo hicho ni cha utumwa, sasa sijui ndo anamlipa kaka diamond coz yeye pia alishawah kufanya hivyo katika show moja iliyofanyika leaders club ya tigo kibokoyao, ukiwa kama mdau wa muziki unasemaje kuhusiana na tukio hilo..?

[PICHAZ] Huu ndo Muonekano Mpya warihana Tizama Pamba anazopiga Akuwa Kitaa... Bofya hapa!!..


Baada ya kuwa aonekani mara nyingi machoni pawatu mwanadada huyu super star Rihanna.

 Aonekana jana asubuhi pande za New York akikatiza katika mitaa na kuingia katika Super Market moja jijini hapo na kufanya mapapalazi kumgoja kwa saa4 mpaka alipotoka na kumpiga picha.

 Akiwapungia baadhi ya watu mikono walio kuwa wakimtizama super star Rihanna


Maeneo ya bataz akiwa anapiga stori na marafiki zake kushoto anaitwa Marry Jackson rafiki yake wa karibu sana.

Je! Umesikia Juu ya habari za Kufo cha John Cena? Ukweli halisi wenye Uthibitisho uko Hapa


Katika siku za hivi karibuni mcheza mieleka maarufu John Felix Anthony Cena amekuwa moja ya wahanga wa mitandao ya kijamii baada ya kuzushiwa kifo.
Habari zimesambaa kwa wingi mtandaoni kuwa Cena amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali ya gari,vyanzo vingine vinadai Cena
amefariki baada ya kuumia kichwani alipokuwa mazoezini na mcheza mieleka mwingine maarufu Dwayne Johnson(The Rock)
Uongozi mzima wa WWE umekanusha habari hizo na kuziita habari zisizokuwa na tija zaidi ya kuzitafutia umaarufu baadhi ya media.
Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top