Inatafuta...

Leo ni Siku ya Mwisho ZEC Kumtangaza Rais..Nini Hatima ya Zanzibar Kuanzia Jumatatu

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar itakapofika November 2 madaraka ya rais aliyepo yatakoma labda baraza la wawakilishi liitishwe kutengua kifungu hicho.

Wakati huo CUF imetoa hadi kesho ZEC wawe wametengua tamko la M/kiti wao na kuendelea kuhakiki majimbo 14 yaliyobaki vinginevyo watawaachia wananchi kudai haki yao wenyewe.
Nini hatima ya Zanzibar kuanzia jumatatu, je Sheni ataendelea kuheshimiwa kama rais au atatafutwa kiongozi wa mpito kipindi cha kusubiri uchaguzi mwingine.

Endapo Dr. Shein ataendelea na madaraka ataaminika vipi kuendelea kupanga uchaguzi wa marudio wakati yeye ni mmoja wa washindani wanaolalamikiwa?

Nawasilisha.

Speed 120 Aliyoihaidi Mh. Lowassa Ingetoka kwa Watu Hawa Kama Angeupata Urais

Edward Lowassa
Ni siku kadhaa zimeshapita ambazo watanzania wengi hasa wale wa mijini waliweka matumaini yao dhidi ya utawala mpya kama nilivyoelezea hapo juu...

Ilikuwa ukipita mitaani utagundua watu wakiwa katika matumaini mapya yenye furaha kuwa hakika yule watakayemchagua ndiye atapita lakini ikawa ndivyo sivyo...

Nilipopita mitaani hasa hapa dar es salaam nilipata nafasi ya kusikia maoni ya watu wengi sana..lakini moja ya maoni ya vijana wengi na wazee wengi pale ubungo kituo cha mabasi yaendayo mikoani ndiyo yaliyonikosha zaidi...

Ni pale niliposikia watu wakidadavua ile ahadi ya lowassa ya speed 120 jinsi ambavyo angetekeleza chini ya baraza hili la mawaziri..kijana mmoja niliyemfahamu kwa jina la yassin alijaribu kuunda baraza la mawaziri chini ya mh. raisi lowassa nalo lilikuwa hivi:::

WAZIRI MKUU----Mh F.A.Mbowe

Waziri wa katiba na sheria---Mh. Tundu lissu.


Waziri wa Maliasili na utalii---Mh. Rev Peter msigwa


Waziri wa wanawake jinsia na watoto---Mh. Halima mdee

Waziri wa ulinzi na usalama---Mh. G.Lema


Waziri wa mambo ya ndani----Mh. J J Mnyika


Waziri wa michezo na sanaa---Mh. Sugu


Waziri wa Waziri wa fedha---mbatia

Waziri wa ardhi----salumu mwalimu


aliendelea kushuka kushuka na akamaliza kwa kusema watanzania mnafikiri chini ya mawaziri hawa kwanini kusiwe na SPEED 120?


SASA: Leo nimepita tena mahali pale Ohooo...ndugu yangu watu kama wamemwagiwa maji....watu wamehuzunika saana watu hawana Amani wamepoteza matumaini hawana hili wala lile....ni sawa na mfungwa aliyewekwa gerezani kwa miaka zaidi ya hamsini baadaya sikuchache akitarajia kufunguliwa halafu siku hiyo anaambiwa ameongezewa miaka mitano tena....ohoooo....piga picha jinsi anatakavyoumia...basi ndivyo hali inavyoendelea huku mitaani....

Hali ni Tete Zanzibar....Bomu Lategwa Kituo cha Polisi, JWTZ Waliwahi na Kulilipua

Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ), limefanikiwa kuteguwa bomu lilitegwa eneo la Mkunazini karibu na kituo cha polisi mjini Zanzibar.

Bomu hilo lilitegwa na watu wasiofahamika na jeshi la polisi lilipata taarifa ya kutegwa kwa bomu hilo kutoka kwa wasamaria wema.

Akizungumza na mwandishi wetu, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame, alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa eneo hilo kuna kitu kimetegeshwa, jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa ni bomu na kufanikiwa kulitegua kwa kuliripua ili kuepusha maafa.

“Ni kweli kulikuwa na kishindo kikubwa baada ya jeshi la polisi kuliripua bomu hilo lakini hakuna madhara yoyote yaliotokea,” alisema.

Aidha alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini ni aina gani ya bomu lililotegwa na aliyefanya kitendo hicho.

Nimeikumbuka Kauli ya DK SLAA "Chama Changu Chadema Hakiwezi Kushinda Urais Mwaka huu 2015 Kutokana na Kula Matapishi Yetu..."

DK Slaa
"Chadema hakikuwa chama cha kukumbatia ufisadi na mafisadi..hakikuwa chama cha kusomba watu na magari mikutanoni...hakikuwa chama cha kuiba na kununua kura...sasa Chadema hii si ile tulioijenga....
nimeamua kustaafu siasa maana najua chama changu hakiwezi kushinda urais mwaka huu 2015 kutokana na kula matapishi yetu..." Dk Slaa:

Je Slaa ni mkweli??

Kwa Wanandoa Tu: Ni Halali Kupokea Simu ya Mumeo/Mkeo Akipigiwa?

In case mumeo/mkeo yuko mbali kidogo na simu yake halafu ikatokea akapigiwa simu na mtu ambaye aidha ni namba ngeni au iliyohifadhiwa kwenye simu, na wewe upo karibu na simu yake, Je, unaweza kumpokelea!
Nawasilisha!

Ni Marufuku Kusafirisha Masanduku ya Kura......Tume Yasisitiza Matokeo Yatatangazwa Vituoni, Fomu za Urais Kuskaniwa Jimboni na Kutangazwa LIVE

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amesema kura zote za urais, ubunge na udiwani, zitahesabiwa katika vituo vya kupigia kura na matokeo yote kutangazwa hapo hapo na ni marufuku kusafirisha masanduku ya kura kama ilivyokuwa zamani.

Jaji Lubuva aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano na wawakilishi wa walemavu   kujadili namna bora ya wao kushiriki katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

Alisema katika uchaguzi wa  mwaka huu ni marufuku kuhamisha masanduku ya kura kwa sababu vituo vya kupigia kura vitabadilika kuwa vituo vya kuhesabia kura baada ya upigaji kura kumalizika.

“Kura zote za urais, ubunge na udiwani zitahesabiwa katika kila kituo na matokeo yatabandikwa vituoni hapo hivyo sijui wanaosema kura zitaibiwa zitaibiwaje,” alisema JajiLubuva na kuongeza:

“Baada ya matokeo kubandikwa katika kila kituo yatapelekwa katika kata husika   kujumlishwa na hapo pia yatabandikwa.

“Mshindi wa udiwani atatangazwa hapo na yale ya ubunge na urais yatapelekwa jimboni ambako yatajumlishwa na mshindi wa ubunge atatangazwa na kukabidhiwa cheti huku ya urais yakipelekwa makao makuu ya Tume.

“Matokeo ya urais yatabandikwa katika kila jimbo na fomu ile ya matokeo itaskaniwa na kutumwa moja kwa moja makao makuu ya tume kwa kupitia mkongo wa mawasiliano wa taifa badala ya simu za mkononi kama ilivyokuwa awali,” alisema Lubuva.

Alisema njia hiyo  itasaidia matokeo kufika kwa haraka kama inavyotakiwa na baada ya tume kupokea matokeo hayo itakuwa ikiyatangaza moja kwa moja kupitia luninga na redio.

Jaji Lubuva alisema  njia nyingine iliyoandaliwa ya kutuma matokeo ni kwa nukushi (fax) ambako  halmashauri zote nchini zimepatiwa vifaa vitakavyoziwezesha kuyatuma matokeo haraka.

Alisema hatua ya tume kutangaza matokeo hayo kupitia luninga na redio itasaidia wananchi kulinganisha matokeo watakayokuwa nayo na yatakayokuwa yanatangazwa na tume.

Kutokana na hali hiyo alivishauri vyama vya siasa viache kauli za kuwataka wafuasi wao wasiondoke vituoni baada ya kupiga kura kwa vile  hakuna kura zitakazoibiwa.

“Sioni haja ya vyama kusema vinalinda kura kwa sababu kura zote zinabaki vituoni na zitahesabiwa palepale tofauti na zamani ambako zilikuwa zikipelekwa kata na jimboni kuhesabiwa,” alisema.

Jaji Lubuva pia alivitaka vyama vya siasa kuacha kuingilia majukumu ya Tume hiyo ikiwamo kuhoji mabadiliko ya watendaji yanayofanywa ndani ya taasisi hiyo.

“Navishauri vyama vya siasa viache kuingilia majukumu ya Tume, haviwezi kutuchagulia na kutuambia pale weka karani fulani hapa fanya hivi… waache kuingia jikoni wasubiri chakula kipikwe watakula kwa haki wala wasiogope,” alisema.

Ametoa kauli hiyo  siku chache baada ya vyombo vya habari kumnukuu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akisema Mkurugenzi wa Tehama wa Tume hiyo, Sisti Cariah ameondolewa katika nafasi hiyo huku akihusisha mabadiliko hayo na maandalizi ya  kuiba kura.

Hata hivyo NEC ilikanusha taarifa hizo   ikisema hakuna mtu yeyote aliyehamishwa katika idara zake zote isipokuwa wakuu hao wa idara walichelewa kuwasilisha picha zao ndiyo sababu  hawajaingizwa katika orodha iliyomo katika tovuti ya Tume.

Jaji Lubuva alisema daftari la mwisho la wapiga kura litakamilika baada ya wiki mbili hadi tatu na wapiga kura watapata fursa ya kulihakiki kwa siku nane kabla ya uchaguzi.

Ukimya wa Mke wa Magufuli Unatia Shaka

Jamani Mke wa Magufuli mbona haonekani kwenye Campaign kama ilivyokua kwa Mama Salma, Mama Anna Mkapa na Mama Regina Lowassa. Kuna nini hapa katikati?

CCM Waituhumu UKAWA Kumwagia Mikojo Ofisi zao Tanga.. Wadai Lowassa Aliahirisha Mkutano Tanga Kwa Sababu Ya Matatizo Yake

Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.
Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani.
Tukio la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri.
 
Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya Taifa letu.
Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi.
Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa.
Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga.
Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana.
 
Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.
Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni.
Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi.

Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote.

Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao.

Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura.
 
Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.
Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015

Ray C akirejesha Umbo lake La Mwanzo Sasa Aongeza Mvuto Picha ziko Hapa..

Huenda jitihada za Ray C kukirejesha kiuno chake kisichokuwa na mfupa zimeanza kuzaa matunda!

Kwa muda mrefu muimbaji huyo amekuwa akijaribu kuupunguza unene wake uliompoteza muonekano wake wa zamani uliompa sifa jukwaani na sasa picha zake mpya zinaonesha mafanikio.

Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, ameshare picha zake mpya kuonesha hatua aliyofikia.

Haka ni kanani???yaani sitaki kuamini haka katoto ni mimi uwiii !jamani nina furaha sana moyoni kumuona ray c.wa miaka ile yaani acha tu!je nipungue zaid au?sasa ndio muda wa kurudi rasmi kwenye muziki Babutale, Mkubwafela dada yenu niko tayari sasa,” ameandika.

Unamuonaje Ray C huyu mpya?

TFF imemfungia Mchezaji Nyoso Kwa Miaka Miwili Kucheza Mpira wa Miguu Baada ya Kumshika Mchezaji Mwenzie Makalio

Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Je wajua ni kwanini Tanzania Itaishinda Kenya kwa kuwa na Ma Milionea wengi? Soma hapa


Why Tanzania Will Soon Overtaken Kenya In Creating Millionaires


Tanzania is creating dollar millionaires faster than any other East African country, a new report says.

This means that East Africa’s newest millionaires are likely to come from Tanzania, as opposed to Kenya, Uganda, Rwanda or Burundi.

According to the African 2013 Wealth Book, the country is ranked third in Africa, after Ethiopia and Angola, with its millionaires’ club growing at a rate of 51 per cent between 2007 and 2013.

While it had 3,700 millionaires in 2007, this number had risen to 5,600 by 2013. Tanzania is followed in the region by Kenya, the only other regional country that features among the top 10 in Africa. Kenya is reported to have had 8,300 millionaires in 2013 against 6,700 in 2007, a growth rate of 24 per cent.

The report, put together by New World Wealth, defines millionaires or high net worth individuals (HNWIs) as those with net assets worth $1 million or more, excluding the value of their primary residences. The survey includes only those countries that had over 800 millionaires in 2013.
On the scale of absolute numbers, Kenya is up there, mixing it up with Africa’s big boys, coming fourth after South Africa (48,700), Egypt (22,800) and Nigeria (15,700).

Tanzania’s faster acceleration must be understood in the context of a country that is coming from a low base.

After decades of a command economy in which the government controlled most of the wealth, the liberalised economy is just warming up and the risk-takers among the population are clearly cashing in. Tanzania is also more resource-rich than its EAC partners.

It is endowed with vast natural gas and oil deposits, besides substantial quantities of gold, diamond and tanzanite. It also has the region’s biggest water and forest resources and is often referred to as the “lungs of the region.”

Thus the newly created millionaires probably individuals who have bet their money on its rapidly developing oil, gas and minerals sector, where massive deposits of offshore gas have made Tanzania a leading investment destination for prospectors and developers. As of June 2013, 42.7 trillion cubic feet of natural gas (about 7.5 billion barrels of oil equivalent) has been discovered in Tanzania.

Tanzania’s gold sector has also witnessed a boom in the past few years, and it is now the country’s leading export, worth $2.2 billion in 2012, followed by tobacco exports at $223 million and coffee at $187 million.

It recorded a growth of 45 per cent between 2007 and 2012 against Kenya’s 20 per cent. Even then, Kenyans were generally richer than their Tanzanian counterparts at a per capita income of $862 against the latter’s $609 in 2012.

In average terms, the richest Africans are to be found in South Africa ($7,508 per capita income), Angola ($5,485), Algeria ($5,404), Tunisia ($4,237) and Egypt ($3,187). While South Africa is known to have a resource-rich and fairly sophisticated economy, Angola is the beneficiary of its oil. The Maghreb countries’ good fortune is a result of a mix of oil and “welfarist” public policies.

Uganda leads the pack in expanding individual wealth in the region. Closer home, Kenya is expected to have 21,200 dollar millionaires, compared with Tanzania’s 15,200.

Mr Akumu writes for the Daily Nation, email – wakumu@ke.nationmedia.com

Mchungaji Peter Msigwa Na Wafuasi 61 Wa Chadema Watiwa Mbaroni

JESHI  la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani  Iringa jana walitumia mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi  zaidi ya 61  wa  chama  cha  Demokrasia  na maendeleo (chadema ) akiwemo mgombea  ubunge wao  jimbo la  Iringa mjini  mchungaji Peter Msigwa   kwa tuhuma za  kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha  kutuliza ghasia (FFU) Iringa na   wananchi  waliokuwa  wakitoka katika mkutano  wa mgombea  Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.

Imeelezwa  kuwa   wafuasi hao ambao  wengi  wao ni vijana walikuwa  wamekutana katika  eneo la kambi ya  kampeni ya Chadema  iliyopo  eneo la Hoteli  ya  Sambala jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa  ajili ya kikao cha ndani toka majira ya mchana na jioni  ndipo  walipofanya  vurugu   hizo  wakati wananchi  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za mgombea  huyo wa Urais wa CCM.

Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi amewaeleza  waandishi wa habari  kuwa tukio  hilo  lilitokea   jana  majira ya saa 12;30   jioni baada  ya  wafuasi hao  kufunga barabara  kuu ya  Iringa –Dodoma  na  kufanya  vurugu  hizo kwa kuwarushia mawe  wananchi  waliokuwa  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za Dr Magufuli uwanja  wa  Samora.

Amesema  kuwa  wakati  jeshi la polisi  likiwa katika mkutano wa mgombea  huyo wa Urais wa CCM walipokea taarifa kuwa  kuna  vijana wa  boda  boda  zaidi ya 150 walikuwa  wakijikusanya  kuelekea  katika eneo hilo la Sambala Lodge  na baada ya kufuatilia ndipo  walibaini  kuwa  wanakwenda katika  kikao chao cha  ndani  na kwa kawaida  jeshi la  polisi halikatazi  watu  kufanya  vikao  vyao vya  ndani .

“Jeshi  la  polisi  halizuii  wanachama wa  chama  chochote cha siasa  kufanya vikao vya ndani kwani  ni haki yao ya  kisheria na kikatiba,lakini  baada ya  kikao chao kumalizika  vijana hao  walitoka  nje ya ukumbi  huo uliopo kando kando ya  barabara na  kuanza  kufunga  barabara  na kucheza muziki katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa barabara

"Baada ya   vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU  kwenda  kuwatoa watu  hao  barabarani ila  walipuuza na kuishia kumpiga mawe  na  baadae  kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya Sambala  eneo  ambalo  wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema  “ alisema kamanda Mungi.

Amesema  wakati wa vurugu  hizo baadhi ya  vijana  waliumia kwa  kuruka ukuta  na wengine kwa  kuanguka wakati wakijaribu  kukwepa  kukamatwa na  kuwa wale  wote waliokamatwa  watafikishwa mahakamani wakati  wowote  kuanzia  sasa na  kuwa miongoni mwao  yumo mgombea  ubunge  jimbo  hilo,Mchungaji Msigwa .

Mbali ya  mchangaji  Msigwa   wengine  waliokamatwa kwa tuhuma  za  vurugu  hizo  ni pamoja na mgombea  udiwani  kata ya  Gangilonga  ambae  pia ni mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo

Hata  hivyo, taarifa  iliyotufikia jion  hii  inaarifu  kuwa Mchungaji  Msigwa  na wafuasi  hao 61  wameachiwa kwa dhamana leo.

PICHA ya Ndege Mbugani Ikionyesha Twiga Akipandiswa Kwenye Ndege...Je nini Kinaendelea ? Ni Photoshoped Au?

Siku ya Leo Kwenye Mitandao ya Kijamii zimesamaa picha zikionyesha ndege ya Nje akiwa Mbugani Huku Baadhi ya Watu wakishughulika Kumpandisha Twiga kwenye ndege hiyo....
Watu wengi Wamelaani kitendo hicho kwa kukumbushia tukio la Twiga Kusafirishwa kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro....

My Take: Nimebahatika kutumiwa picha hii hapa chini ambayo inafanana na hiyo hapo juu bila kuwa na hiyo picha ya Twiga na hao watu Wakimshusha Twiga Kwenye Gari...kitu ambacho kwa Haraka Haraka inaonyesha Picha  ya Juu ni Photoshoped......

Mdau Embu Angalia na wewe hizo picha mbili na Utoe maoni yako....

Shamsa Ford: Nataka Mabadiliko.....Siwezi Kujidhalilisha Kufuata Fedha CCM

Staa wa  filamu ya Chausiku, Shamsa Ford amesema hatobadilisha msimamo wake wa kushabikia vyama vya upinzani kwa kulaghaiwa na wasanii wachache kwa maslahi yao binafsi .

Shamsa amesema hayupo tayari kufuata maamuzi ya watu wengine hata kwa lundo la fedha kwani  kufanya hivyo  ni kujidhalilisha .
Mimi nitabaki huku kwa kuwa nahitaji mabadiliko,kila siku wasanii tunalia tukidai tunaibiwa na hakuna utekelezaji na matokeo yake tunapewa ahadi zisizoisha.”Amesema Shamsa

Aidha , Shamsa Ford aliwataka mashabiki kuwaona kama watu wakawaida kwani baada ya siasa maisha yataendelea kama zamani.

Magufuli Aigeuzia Kibao Taasisi ya Utafiti Iliyompa Ushindi wa Urais..Adai Amepunjwa Asilimia

Kahama. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema waliofanya utafiti wamempunja asilimia kwani ana uhakika wa kushinda kwa asilimia 95 na si 65 kama zilivyotajwa kwa kuwa wananchi wanampenda, naye yuko tayari kufanya kazi ili kuwaletea maendeleo.

Akizungumza jana mjini Kahama, Dk Magufuli alisema: “Wapo wanaosema nimeshinda kwa asilimia 65, mimi ninasema nitashinda kwa asilimia 95, ninachoomba mjitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ili nitangazwe mshindi, ninawaahidi kwamba nitawatumikia na kujenga Tanzania mpya.”
Hivi karibuni, taasisi ya Twaweza ilitoa utafiti wake uliompa nafasi ushindi wa asilimia 65 huku mpinzani wake, Edward Lowassa akipata asilimia 25 na mgombea wa ACT –Wazalendo akipata asilimia 0.3.
Baadaye, taasisi ya Ipsos (Synovate) ilitoa utafiti wake ukionyesha kwamba alishinda kwa asilimia 62 huku Lowassa akipata asilimia 31 na Anna Mghwira akipata asilimia 0.3.
Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top