Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia
ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la
Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City
kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi
milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji
alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Post a Comment