Inatafuta...

Kijana Henry Chau achinja familia yake na kuwala Nyama.. Habari kaili iko hapa..



http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/04/01/150401055530_chau_kiliing_512x288_bbc_nocredit.jpg Henry Chau anayejiita mwendawazimu
Mwanamume mmoja raia wa Hong Kong amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji,kutawanya viungo vya nduguze ,kuwanyunyizia chumvi na kuwapika.

Mtuhumiwa huyo wa mauaji ya kushangaza ana umri wa miaka thelathini na mmoja jina lake ni Henry Chau aliibua hisia za walio wengi katika kesi ya namna yake mnamo 2013 wakati kichwa cha mamake mkubwa pamoja na babake vilipobainika kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.

Majaji wa mahakama kuu nchini Hong Kong ,wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea walisikiliza namna Chau alivyotekeleza mauaji yake ,kwanza huua, pili hutawanya viungo vya maiti na kisha huwanyunyizia chumvi ili kuongeza ladha ,na anasema yote hayo ni matokeo ya mapenzi yake kwa nyama choma ya kiti moto,na nyama hiyo ya binaadamu zikisha iva ama kuchomwa huwa anafunga nyama hizo katika makasha ya chakula paoja na ubwabwa,na polisi walipofanya upekuzi katika nyuma yake walikuta baadhi ya viungo katika chombo cha kuhifadhia taka.

Akitoa hukumu dhidi ya kesi hiyo,jaji Michael Stuart-Moore alimuelezea Chau kama mbinafsi mwenye msongo wa mawazo kutokana na mafanikio mabaya yake ya maisha na asiye na huruma kwa wengine.

Chau, alihukumiwa adhabu mara mbili kifungo cha maisha jela na miaka tisa namiezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa kuvunja sheria ya kuzika miili ya familia yake isivyo kawaida kosa ambalo alikiri baadaye.

Rafiki wa Chau anayehusishwa katika mauaji hayo alikutwa hana hatia mwishoni mwa wiki iliyopita .

Taarifa za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa ,Chau alidanganya kuwa jamaa zake walikwenda China,lakini baadaye alijisahau na kumuandikia rafikiye kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.

Chau mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia watu wake wa karibu na kusema kwamba hawezi kumuonea huruma mtu yeyote kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni mpaka anakuwa mtu mzima.Na alimua kuwadanganya polisi ilia pate wasaa wa kuwaaga marafiki zake.

Changia Maoni Yako Hapa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top