Inatafuta...

Lulu: Ifike muda tutumie mitandao ya kijamii kusaidiana mawazo na sio kutukanana

Moja ya mambo sita tuliyoandika kuwa ni sababu ya watanzania kuupenda mtandao wa Instagram, ni kushuhudia matusi ambayo mastaa wanayavuna kutoka kwa followers wao.

Lakini unadhani Instagram inapaswa kuwa sehemu ya kihuni kiasi hicho? Hapana.

Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael anaamini hawezi kufikia malengo yake kwa mawazo yake pekee bali anahitaji msaada kutoka kwa vijana wenzake ambao nao wana nia na malengo kama yake katika kufikia ndoto zao. Ndio maana anahisi Instagram inaweza kuwa ni sehemu nzuri ya vijana kupenda michongo na sio matusi.

Nikiwa Kama Kijana Mpenda Maendeleo, mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu peke yangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka,” ameandika kwenye Instagram.

Najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii Kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo Ili wote tuweze Kuwa sehemu fulani siku moja.”

Lulu ameonesha wazi kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya hasa kwa kudhalilishana.

Changia Maoni Yako Hapa

3 comments

Safi... Inaonesha Umekua sasa eeeh?..

Reply

Ujumbe Mzuri shukrani

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top