Staa mrembo kutoka Bongo
Movies,amewaasa wanawake kuacha kutoa mimba hata kama watakumbana na
mtatizo,kwani mtoto ndio kila kitu katika maisha.
Msanii huyu alitoa wito huo
hivi juzi kati akiwataka wajawazito wote waliokataliwa na wapenzi wao
kuonyesha kuwa wao ni wanawake majasiri kwa kutothubutu kutoa mimba
hizo.
‘Mtoto ni zawadi kutoka
kwa Mungu, siku ya leo nawashauri wanawake wanaokataliwa mimba na
wapenzi wao wasitoe wala kufanya chochote muonyeshe kama wewe ni
mwanamke jasiri na unaweza, mtoto ndio kila kitu, ‘plzzzz’ usitoe
mimbaaa’. Alisema.
Kufuatia ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionekana kumuunga mkono mrembo huyu ambae ni mama wa mtoto mmoja
Post a Comment