Inatafuta...

Aunt Ezekiel Anaswa Kliniki Akiwa Kapiga Kininja Ushahidi uko hapa!!..

Mama kijacho ambaye ni msanii wa filamu, Aunt Ezekiel juzikati alinaswa akiwa  kliniki huku akiwa amevaa vazi la baibui ambalo linamuonesha macho tu, maarufu kama vazi la kininja.
 
Msanii wa filamu, Aunt Ezekiel akiwa amevaa vazi la baibui ambalo linamuonesha macho tu, maarufu kama vazi la kininja.
Paparazi wetu akiwa kwenye majukumu yake, ghafla alimuona staa huyo ambaye ni wa kujifungua leo au kesho akiwa kwenye vazi hilo katika Hospitali ya Penisulla iliyopo Msasani jijini Dar, hali iliyosababisha watu kutomtambua.
Hata hivyo, wakati akitoka kwa daktari, mwandishi wetu aligundua kuwa aliyekuwa akimuona mbele ya macho yake ni Aunt na ndipo alipomfuata na kumuuliza kulikoni.“Nimechoka kuangaliwaangaliwa, yaani mimba yangu imekuwa kama kitu cha ajabu, kila ninapopita watu macho kodooo, ndiyo maana nimeamua niwe navaa hivi ninapokuwa kwenye maeneo  yenye watu wengi,” alisema Aunt.

Changia Maoni Yako Hapa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top