Askofu wa Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima
amelitikisa tena Jiji la Dar es Salaam leo mara bada kuwasili
makao makuu ya Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili
kuendela na mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu Askofu Pengo.
Gwajima amewasili leo Kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku
akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama
pamoja na Mwanasheria wake .
Eneo lote la kituo hicho cha polisi lilikuwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
Eneo lote la kituo hicho cha polisi lilikuwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
Baada ya kuwasili kituoni hapo, umati mkubwa wa
Waumini wake ulizunguka maeneo yote ya Kituo hicho huku wengine
wakiwa maeneo ya stendi ya Treni ya Reli ya kati.
Kama kawaida, Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa mahususi kumpa nguvu Askofu huyo ajipu kesi hiyo kwa ufasaha.
Kama kawaida, Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa mahususi kumpa nguvu Askofu huyo ajipu kesi hiyo kwa ufasaha.
Baada ya Mahojiano ya takribani masaa Matano,
hatimaye Askofu Gwajima alitoka ndani ya kituo hicho,lakini
katika hali isiyo ya kawaida,Askofu huyo aligoma kuongea na vyombo
vya habari.
Baada ya Gwajima kugoma kuongea,mwandishi wetu
alimfuata Mwanasheria wake aliyekuwa ameambatana naye,Paul
Mallya ambaye alisema kuwa mteja wake alikuwa amechoka, hivyo
asingeweza kuongea.
Mallya alimweleza mwandishi kuwa mambo aliyohojiwa
Gwajima leo ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu
Pengo.
“Askofu kahojiwa maswali mengi tena sio ya kuhusu
kumtukana Askofu Pengo.Wametaka hati ya Helikopta yake anayomiliki,hati
za kanisa lake na hati za viwanja vyake ambavyo ameambiwa
avipeleke wiki ijayo,” alisema Mwanasheria Mallya.
Mallya aliongeza kuwa kutokana na Afya ya mteja wake kuwa mbaya , mahojiano yake yameahirishwa hadi wiki ijayo.
1 comments:
Duuuh! Atazimia Jamani Muacheni
ReplyPost a Comment