MDADA mwenye figa namba nane kunako gemu ya Bongo Fleva, Meninah, jana ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa (birthday) kwa aina yake katika viwanja vya Hekima Garden vilivyopo Mikocheni B jijini Dar.
Katika birthday hiyo wasanii kadhaa wakiwemou Kadjanito, Shilole, Nuh Mziwanda, JI na Queen Darleen walikuwepo kumpa sapoti ya nguvu msanii mwenzao huyo katika sherehe hiyo iliyopambwa na mbwembwe kibao. Miongoni mwake ni keki zilizokuwa na maumbo ya piano na gitaa na kisha kufuatia shoo kali kutoka kwa mwanadada huyo.
Post a Comment