Afya ya mama mzazi wa msanii nyota wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz, Sanura Kassim ‘Sandra’
bado si shwari juzikati hali yake ilibadilika ghafla na kuilazimu
familia yake kumkimbiza katika Hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini
Dar ambako amepewa kitanda, Ijumaa limetonywa.
Chanzo cha uhakika kililieleza gazeti hili kuwa mama Diamond ambaye
amekuwa akisumbuliwa na maradhi yenye kuashiria kupooza, juzikati
alizidiwa na kusababisha ndugu zake wampeleke hospitali
“Mamake Diamond ana wiki sasa hospitalini, lakini mwenyewe Diamond
hataki watu wajue, anakwenda kwa kujificha, wakati mwingine hadi saa
saba usiku, sijui anaficha nini wakati suala lipo wazi tu, nadhani
tukeshe tukimuombea ili hali yake iweze kurudi kama zamani,” kilisema
chanzo chetu.
Gazeti hili lilifunga safari hadi hospitalini hapo ili kujiridhisha
juu ya habari hizo, lakini mhudumu mmoja aliyeulizwa juu ya uwepo wa
mama huyo, alikubali kuwa ni kweli amelazwa hapo, lakini lisingeweza
kuruhusiwa kumuona bila ruhusa ya Diamond au wanafamilia.
Diamond alipotafutwa kuzungumzia afya ya mama yake aligoma kusema
lolote zaidi ya kuomba aachwe kwani wanao uwezo wa kuzungumzia mambo
mengine bila kugusia kuhusu mzazi wake.“Naomba unipe muda maana nina
matatizo sana, hata kuzungumzia ishu hiyo nadhani hakuna haja,” alisema
Diamond.
Inatafuta...
Post a Comment