![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi941bPJhTTi4O6sGY5kMxKsp5bUCgoSpxNHAYYcHU5M0xQkST2MIz00vgHJ2gfonObLtGVdhN2r9CUqy29IAwDkHv9ikYbQ-QulaFNG_kPWdMdWoaT0lBuniQvVyPCuiiBjdrcZY1aKcel/s1600/mabibo.png) |
Mwanafunzo wa Chuo Kikuu Kitandani |
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , Cecilia Mosha (26)
aliyejirusha kutoka ghorofa ya tatu hadi chini kutokana na hofu ya moto
uliotokea katika Hosteli ya Mabibo, amevunjika mfupa wa bega. Mwanafunzi
huyo alijirusha kupitia dirishani juzi katika harakati za kujiokoa na
moto baada ya jengo la wasichana, Block A kushika moto.
" Nilisikia kelele za moto nikiwa chumbani na nipotoka nje nikakuta
moshi umetanda kila kona, baada ya kuona hivyo niliona ni vema nijiokoe
kwa kujirusha kutoka ghorofa ya tatu ya bweni hilo hadi chini kupitia
dirishani,” amesema Cecilia Mosha
Tupia neno moja kumtakia afya njema huyu mwanafunzi.
Changia Maoni Yako Hapa
Post a Comment