
Na Chalila Kibuda ,Globu ya jamii
Jeshi
la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linaendelea na uchunguzi dhidi
ya Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
Dk.Wilbrod Slaa anayedaiwa kufanya njama ya kumuua kwa sumu, Bw. Khalid
Kagezi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishna Suleiman Kova amesema wamechukua maelezo kwa Katibu
Mkuu Dk.Wilbrod Slaa pamoja na maelezo ya mlizi wake Khalid Kagezi.
Kamishina
Kova amesema Chadema walichukua hatua mbalimbali na kujiridhisha
kuhusika kwa mlinzi wa Dk.Slaa kufanya mikakati ya kumuua kwa sumu kwa
kuiweka katika maji au chakula.
Amesema
kwa maelezo ya Mlinzi huyo alidai kuteswa na baadhi ya watu wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwataja kwa majina.
Kamishina
Kova amesema Kagezi alidai kutekwa na kushambuliwa katika mwili wake na
jeshi la Polisi likampa fomu namba tatu (PF3)kwa ajili ya matibabu
“Jeshi
la Polisi limefanya jitihada kwa kupata maelezo kwa watu wote ambao
wamehusika kwa mlizi na Dk.Slaa”amesema Kamishina Kova.
Amesema baada ya uchunguzi watapeleka kwa wakili wa serikali na yeyote atakayehusika sheria itashika mkondo wake.
Wakati
huo huo, Haroub Mtopa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kufanya
utapeli katika ofisi ya Rais kwa kudai kuwa yeye ndiye Katibu wa Rais
Bw. Prosper Mbena.
Mtopa
amekamatwa jana baada ya kutegeshewa mtego wa sh.250,000 za jeshi la
polisi kwa mtu anayedaiwa kutapeliwa kutaka kumuongeza fedha kwa mara ya
pili.
Kamishina
Kova amesema Mtopa alikuwa kila siku anapita Ikulu kwa matatizo
mbalimbali kumbe ndio alikuwa akiwatega watu na kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu.
Amesema watu wanaofika katika ofisi zote bila kuwa na taarifa zao wawafatilie kutokana na kufanyia utapeli kupitia ofisi hizo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo.
Post a Comment