Inatafuta...

Ommy Dimpoz:Diamond si yupo na Zari au? Sidhani kama amemind mimi kufanya kazi na Wema

Mwanamziki Ommy Dimpoz ameyasema hay oleo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokuwa anautambulisha wimbo wake wa Wanjera ambao mrembo Wema Sepetu amecheza kama Wanjera kwenye video wa wimbo huo na kushiriki kupiga picha za kuutangaza wimbo huo.

Ommy alisema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo licha ya Diamond kutoandika chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.

 “Labda hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au? Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”

Changia Maoni Yako Hapa

3 comments

Mapenzi yanakupelekesha Dimpos uspoangalia tutakusahau

Reply

Sawa sawa Baba Nyimb nimeikubali kazana,, Aidia ya video iko poa sana

Reply

Hivi nyie niwapenzi Au mnatuzingua tu maana hatuwaelewi!!!!!!!

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top