Inatafuta...

[URAIS] Lowasa Aoekana Kuwa Na Nguvu Kuliko Chama. Wafuasi wazidi Kuongezeka...

kikwete_lowasa_monduli (1)
Historia ya 2005 ccm "kujirudia"
Ni Katika harakati za kuusaka urais, chaguo la Mkapa lilikuwa Sumaye, lakini nguvu na mtandao uliotengenezwa na timu Kikwete ukiongzwa na Striker Lowassa pamoja naye Rostam, vilimtisha Mkapa hata akaachia taratibu zisizozoeleka Ccm kuchukua mkondo wake hatimae Kikwete akapitishwa kugombea Urais,
Leo hii Kikwete amesahau, na wala hakumbuki kuwa bila nguvu hiyo (Ya Lowassa) asingekuwa Magogoni pale, 

"Prof Kikwete " yeye chaguo lake ni 'vijana' kila siku anajinasibu hivyo kwa kuwahamasisha vijana kujitokeza kuwania urais, na wala hataki kabisa kuzungumzia nguvu na uwezo wa Swahiba wake.

Mbinu ile ile aliyoiandaa Lowassa kumsafishia njia Kikwete, Leo hii kijiti ni Chake, anapanga mashambulizi mazito, yeye mwenyewe, Mara utasikia Maaskofu waandamana kumwomba Lowassa agombee, Mara walemavu, Mara wanafunzi Mara wazee Sijui wa wapi! Yaani ni shiiida na vurugu mechi,
Pamoja na nguvu na uwekezaji mkubwa wa Membe au wapigania urais wengine, hakika Urais mwaka huu ni mgumu, kupitia Ccm hapatatosha kabisa, ngoja tusubiri jeuri ya Ccm kumkata Lowassa, maana jamaa amejiapiza, 'Jua lichwe lisichwe, Mvua inyeshe isinyeshe, liwake lisiwake, lazima agombee urais kwa njia yoyote (tusubiri).
Kwakuwa mhusika wa urais ni yeye mwenyewe ndiyo maana nasema historia ya 2005 itajirudia, Kikwete (mwenuekiti wa chama) lazima abadili maamuzi ya msimamo wake kuhofia kishindo cha Lowassa, Je unadhani ccm wataweza kuzuia upepo wa Lowassa?

Changia Maoni Yako Hapa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Bongo Choice | Modified By Bongo Choices
Back To Top