Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza
na kusema kuwa hata yeye anampa pongezi mpenzi wake wa zamani, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kwa jitihada alizozifanya mpaka kufikia hatua ya
kumaliza nyumba yake iliyopo Madale jijini Dar.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wema alisema kuwa hata kama hawako pamoja lakini kama kuna kitu cha kumsifia kwa jambo zuri alilofanya hana sababu ya kukaa kimya na akinyamaza atakuwa mnafiki.
“Nikikaa kimya bila ya kumpongeza Chibu nitakuwa mnafiki, amefanya jambo zuri la kuigwa hivyo binafsi nampongeza kwa hapo alipofikia,” alisema Wema ambaye katika hatua za mwanzo za ujenzi huo alishiriki.

1 comments:
Wema unazidi kunikosha mamaa,,, hunakinyongo na m2
ReplyPost a Comment