Kama wewe ni mmoja kati ya watu waliochukizwa au kuumizwa na taarifa
kuhusu ndoa ya mastaa wawili wanao make headline kwa sasa, zarinah
hassan aka zari pamoja na mpenzi wake diamond platnumz, taarifa ikufikie
kuwa uvumi huo haukuwa kweli, diamond na zari "HAWAJAFUNGA NDOA"
Uvumi huo ulienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, mara baada ya
mastaa hao kupiga picha wakiwa wamevaa mavazi ya harusi na kuzitundika
kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa zinasema picha hizo zilipigwa mahsusi kwa ajili ya kuitangaza
shoo kubwa ya super star kutoka uganda, ZARINAH HASSAN . Show hiyo
inayotambulika kwa jina la CIROC ALL WHITE PARTY ambayo itafanyika
kwenye ukumbi mkubwa pale MLIMANI CITY mei moja.
Zile picha walipiga kwa ajili ya kuitangaza show hiyo kubwa
inayotabiriwa kuvunja record kwa kuhudhuriwa na mastaa pamoja na watu
mbali mbali mashuhuli.
Post a Comment