Dakika kadhaa tu baada ya kifo cha Abdu Bonge, msanii wa TipTop
Connection Tunda Man alipost picha kwenye account yake ya Instagram
akiwaambia mashabiki wake wa Kenya wakae tayari kwa show yake akisema ‘Pande za 254 kitawaka mbaya pale jamboree Mombasa, watu wa Mombasa tukutane palee‘
Ni post ambayo ilifanya mashabiki wengine wamtukane, wengine wamlaumu na
wengine wahisi kama aligombana na Tiptop hivyo hana shughuli na
yanayoendelea kwao ambapo pamoja na hayo, Tunda Man amesema wote hao
hawakuwa wanaujua upande wa pili wa picha hiyo, yani kilichotokea hasa.
Akiongea akiwa analia Tunda Man amesema >>> ‘Abdu
Bonge ndio aliipost hiyo picha mimi nilikua naendesha gari manake
alikua anajua mimi nilikua natakiwa kwenda Mombasa wiki hii, simu
haikuwa na hela kwa hiyo baadae nilipoweka pesa ndio ikajipost wakati
nikitaka kuweka picha ya Marehemu, ilivyojipost ikabidi niende nikaifute
nikaweka nyingine’
‘Ni
mtu ambae nilikua napiga nae picha nyingi na huwa anazipost mwenyewe,
ana comment sababu anajua mimi ni mzembe naweza nisiwe nakumbuka kupost
kuhusu kutangaza show zangu, bila Abdul Bonge sidhani kama kuna mtu
angemjua Tunda Man sasa hivi
2 comments
Pole sana kaka!
ReplyMi nilimporomoshea vitu, Nliona sasa huyu jamaa kachanganyikiwa sasa...
ReplyPost a Comment