MREMBO anayekimbiza na ngoma ya Ulithemba,
Esterlina Sanga ‘Linah’, juzikati alifunguka kwamba, wivu wa mchumba
wake Nangari Kombo ‘Nanga’, nusura umkoseshe mamilioni ya fedha
alizopewa kwenye udhamini na Kampuni ya Serengeti.
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Esterlina Sanga maarufu kama ‘Linah’.“Nimeamini wivu ni adui mkubwa wa maendeleo kwenye maisha maana kama usipoweza kuuzuia unaweza kujikuta ukishindwa kutimiza ndoto zako kama ilivyotaka kunitokea kwani kila mara nilipokuwa nikiongea na bosi wa Serengeti mchumba wangu alikuwa akinikoromea hivyo kama ningemsikiliza nisingepata hili dili,” alisema Linah.
Source : GPL
Post a Comment