
Mtoto
wa miaka 2 aweka rekodi India Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka
miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini
India.
Kulingana
na vitabu vya kumbukumbu ya rekodi za taifa, Dolly Shivani Cherukuri
kutoka Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh aliweka rekodi ya kuwa
mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kusajili alama 200 katika mashindano
yaliyoandaliwa jumanne iliyopita.
Kulingana
na jarida la Press Trust la India ,mtoto huyo alifuma mishale 36 kutoka
umbali wa mita 5 na kisha umbali wa mita 7 na kujizolea alama 388.
Tukio
hilo lilishuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya
kumbukumbu za michezo.''kwa hakika tunajivunia matokeo haya ''alisema
afisa wa shirikisho la mishale la India bwana Gunjan Abrol.
Dolly ambaye alizaliwa baada ya kupandikizwa kwa mbegu ya babake kufuatia kifo cha kakake katika ajali ya barabarani.

Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India.Kakake alikuwa mrushaji mishale wa kimataifa Cherukuri Lenin.
Babake Cherukuri Satyanarayana ,anasema kuwa Dolly alifunzwa kufuma mishale, tangu alipozaliwa.
Babake ni mmiliki wa klabu kimoja kinachofunza kurusha mishale.
Aidha
aliiambia shrika la habari la AFP kuwa kitambo alikuwa amemptengezea
uta na mishale nyepesi ilikukuza talanta ya mtoto huyo.
Sasa
babake anasema kuwa anapanga kumshirikisha mwanawe katika mashindano
kwa nia ya kumsajili katika vitabu vya rekodi za dunia za Guinness.
BBC
Post a Comment