Wema Sepetu akiwasha gari Jipya la ASX Mitsubishi katika uzinduzi wa gari hilo jijini Dar es Salaam.
Hili ndilo gari la ASX Mitsubish jipya lililozinduliwa wiki iliyopita katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam
Millard Ayo, Wema wasifia gari jipya la 2015 Mitsubishi ASX.
Mtangazaji
wa Clouds FM, Millard Ayo na mwigizaji maarufu nchini, Wema Sepetu
wamesifia gari jipya la Mitsubishi ASX la mwaka 2015 linalouzwa na
kusambazwa na kampuni ya Diamond Motors (Hansa Group).
Katika
uzinduzi wa kutambulisha gari hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine Kampuni ya Diamond Motors
wauzaji pekee wa magari kutoka Mitsubishi waliwaalika Millard Ayo na
Wema Sepetu kujaribu gari hilo toleo jipya Mitsubishi ASX kabla ya
uzinduzi.
Mastaa
hao walivutiwa na mwonekano wa Mitsubishi ASX lenye vioo vya kisasa juu
vyenye mwanga unaomwezesha dereva na abiria kufurahia mwonekano wa
pande zote.
Meneja
mauzo wa Diamond Motors, Reena Ganatra alisema Gari hilo lenye luninga
ndogo inayocheza DVD, iPods, Bluetooth na sauti kutoka vyanzo mbalimbali
ni maalumu kwa vijana wa kisasa na familia kwani Mitsubish ASX
limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye kulifanya liwe na nguvu ya
150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa mwendokasi mkubwa na
kwamba limetengenezwa maalum kutumia mafuta kidogo.
“ASX
ni mwanzo tu, tunazo aina nyingine za magari kama kama Pajero ambayo
tunakaribia kuyatambulisha sokoni ili kuwapatia watanzania magari imara
na yenye kuaminika kutoka Mitsubishi” Alisema Ganatra.
ASX
toleo la 2015 limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu na imara likiwa na
bodi gumu pia lina mfumo maalumu usiotegemea funguo hivyo kumfanya
mwendeshaji kuwasha injini kwa kubofya kitufe.
“ASX
kutoka Mitsubishi, imetengenezwa maalumu kukidhi mazingira ya Tanzania
hasa mijini kama Dar es Salaam ambapo muda wowote dereva wa kawaida
anatoka kwenye barabara nzuri na kuingia kwenye barabara zenye
makorongo” alisema Ganatra
Injini
ya gari hilo ambayo ni 2.0-liter imeunganishwa INVECS-III CVT
inayoisaidia mwendelezo wake katika kubadili mwendo pamoja na uimara wa
usukani unaosaidia mikono ya dereva kuwa salama hata anapokuwa katika
mwendo mkali.
Post a Comment